Tuesday, August 21, 2012

TUSIHARIBU SENSA KWA MITAZAMO YA DINI ZETU, TUSHIKAMANE KAMA WATANZANIA - Samora Julius


Kwanza kabisa ningependa kutoa wito wangu kwa watanzania kushiriki kwa ustadi na umakini wa hali ya juu katika zoezi zito na muhimu katika taifa letu ambalo si lingine bali ni sensa.

Ndugu watanzania, hakuna kitu muhimu kama kushiriki katika shughuli ya kupanga maendeleo yetu wenyewe, kushiriki katika sensa ni kuonyesha uzalendo wako katika taifa lako. swala la sensa si Tanzania tu ni bali ni swala la NCHI ZOTE na umuhimu wako hujikita katika mambo makuu kama matatu hivi nayo ni:

(1) kuangalia hali ya uchumi na ustawi wake wa jamii.
(2) kutayarisha mipango ya maendeleo.
(3)kuweka misingi itakayosaidia kufanya maamuzi.

Ndugu watanzania, kuna mawazo machafu yanayoenezwa na watu au kikundi cha watu kuwaada watanzania kutoshiriki katika zoezi la sensa hapa napata HOFU tena kubwa kwa mtanzania huyu anafanya hivyo kwa manufaa ya nani na kwalengo gani?

Tukianza kujitambua kwa DINI zetu katika zoezi hili la sensa basi tunapotaka kuelekea ni pabaya sana maana tukitoka kwenye kutambuana kwenye DINI tutaamia kwenye madhehebu yetu kwamba hawa ni wengi kuliko wale,tukishamaliza kwenye DINI tutahamia kwenye makabila yetu. Ndugu zangu tuwe makini JUU YA JAMBO HILI LA SENSA NA DHANA YA UDINI.

Tukumbuke sisi ni watanzania na tutabaki kuwa watanzania bila kujali makabila wala dini zetu, swala la sensa lisije likawa kama chanzo cha kuvuruga amani tulionayo maana kuna watu wachache wanaotaka kutuvuluga watanzania katika mambo muhimu katika maendeleo yetu.

Ifahamike kwamba SENSA ni kama moja wapo ya nyenzo muhimu katika kupanga na kujitasmini sisi kama watanzania wapi tumetoka na wapi tunapotaka kuelekea si kwa manufaa ya watu au kikundi cha watu wachache na bila kuangalia DINI zao au makabila au sehemu wanazotoka.

WITO WANGU KAMA MTANZANIA NISIYEJITAMBULISHA AU KUJIPAMBANUA KWA KABILA au DINI YANGU NAPENDA KUWASIHI WATANZANIA KUSHIRIKI KWA MOYO MMOJA KATIKA ZOEZI LILILOPO MBELE YETU KWA KUJITAZAMA KAMA MTANZANIA NA SI VINGINEVYO.

MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRIKA

1 comment:

  1. Jamani!
    Huu ni wakati wa kuwa makini sana na watu ambao kwa ufinyu wao wa mawazo wanaweza kuleta maafa makubwa sana katika taifa hili, Ukisoma katika Biblia utaona Musa akiwahesabu wana wa Israeli na pia utamuona Yoshua akiwahesabu waisraeli kabla ya kuvuka mto Yordani, na hawa wote waliwahesabu wana waIsraeli kwa maagizo maalum ya Mungu Mkuu, Ikiwa hawa ndugu waislaamu wanamuamini Musa kuwa ni nabii wa Mungu na ikiwa mambo aliyoyafanya Musa yapo bayana je, hili jambo wamelitoa wapi? na ni misingi gani wanayoitumia kupinga jambo hili? Mbona kuna wenzao wanaowashangaa? watu wa aina hii(wapinga sensa) ni hatari sana ni wapinzani wa kila jambo hata la maslahi kwao na wanatakiwa wafunguliwe fikra zao...maana ni hatari hata kwa dini zao. Ni wapingajiii hawana jipya,
    SWALI:
    1. Je huwa hakuna daftari ya kumbukumbu misikitini mwao ili kujua idadi ya waumini wa msikiti husika?
    2. Nakumbuka mwaka fulani walisema kuwa wao ni wengi kuliko wakristo, Je, walitumia kugezo gani kujua hili?

    Mbona wanatunganya kwa hadithi zao za sungura na fisi? waombewe hawa fahamu zao zifunguke.

    ReplyDelete

JENGO LA KANISA TAG CITY HARVEST LAWEKWA WAKFU RASMI

HATIMAYE jengo Kanisa la TAG City Harvest limezinduliwa na kuwekwa wakfu na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, Rev. Dk. Barnabas Mt...