Askofu Mtokambali alisisitiza juu ya sifa za nyumba ya Bwana ambazo ni Utakatifu, Maombi, Uponyaji, Sifa (Mahali pa Kusifu) na Kushinda Vikwazo; akihubiri kutoka kitabu cha Mathayo 21:12-17.
Uzinduzi huo wa City
Harvest uliambatana na maadhimisho ya kutimiza miaka saba ya tangu lianze kutoa
huduma za kiroho katika jiji la Dar es Salaam.
Tangu Februari, mwaka
2011, Kanisa la City Harvest limeendelea kukua na kupanua wigo katika kutimiza
malengo yake hasa kuwasaidia wanataaluma vijana na wanafunzi wa vyuo vya elimu
ya juu.
Muasisi wa City
Harvest, Mchungaji Kiongozi, Architect Yared Dondo alipata maono ya kuanzisha
kanisa hilo kwa lengo la kuwasaidia vijana wa vyuo kupata uelewa kuhusu masuala
ya kiroho na kitaaluma na kuwafikia wanataaluma wenzao kwa Injili ya Kristo.
Mchungaji Dondo ambaye
ni Msanifu wa Majengo (Architect) alipata maono hayo wakati akisimamia mradi wa
ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) miaka ya 2007/8.
Katika kipindi hicho, Mchungaji
Dondo alishuhudia vijana wengi waliokuwa wanawasili katika eneo la chuo hicho
kwa mara ya kwanza, ili kuanza masomo, lakini hapakuwepo na eneo maalum la
kuwasaidia vijana kukusanyika kwa ajili masuala ya kiroho kama kuabudu na
kumsifu Mungu.
“Niliwaangalia
wanafunzi wale wanaingia na mizigo yao wakiwa na nyuso zilizojaa matumaini ya
kuanza maisha mapya, kuvumbua mambo mapya na kupata taaluma na bila shaka
maisha bora,”
“Moyo
wangu uliugua, niliwaza jinsi ambavyo maisha ya Chuo bila Yesu yana mashaka
mengi sana. Nikaona jinsi ambavyo rasilimali hii muhimu kwa wazazi na
taifa imepotea bila Yesu,” anaelezea
mchungaji Dondo.
Historia ya City
Harvest
City Harvest lilianzishwa
Februari 20, 2011, katika ukumbi wa sinema uliopo Mlimani City jijini Dar es
Salaam.
Akielezea changamoto
walizozipata pindi wanaanzisha kanisa hilo, Mchungaji Dondo anasema katika
kipindi hicho kulitokea changamoto ya aina yake kwani awali walipata ukumbi kwenye
jengo lingine, lakini baadae walipata taarifa kutoka kwa uongozi kuwa, jengo
hilo haliwezi kutumika katika masuala ya kidini, ikiwa ni siku mbili kabla ya
ibada ya kwanza kabisa kufanyika.
“Ilikuwa changamoto
kubwa, kwa sababu maandalizi yote yalikuwa yamekamilika, lakini Mungu
alituwezesha kupata ukumbi huu wa sinema ingawa gharama ilikuwa kubwa, tukaona
tufanye angalau ufunguzi na mambo mengine yatafuata,” anasema.
“Kitu ambacho sitaweza
kusahau katika maisha yangu, ni siku ambayo ukumbi wa watu 250 ulijaa na watu
wakakaa mpaka kwenye ngazi (steps), wakiwemo watoto wengi; pamoja na kuwa
tulibadili sehemu ya kukutania muda wa mwisho”
Kwa kipindi cha wiki 70,
sawa na mwaka moja na nusu, City Harvest ilikuwa inalipa kiasi cha Tsh 900,000/-
kwa saa tatu kila Jumapili kwenye ukumbi huo wa sinema.
Mchungaji Dondo anasema
gharama ya kukodi ukumbi ilikuwa kubwa kumudu lakini sadaka ya Jumapili ya
ufunguzi katika ukumbi wa sinema ilitosha kulipa gharama za pango siku hiyo na
jumapili iliyofuata. Tulimshangaa Mungu
“Mungu aliendelea
kutushangaza hivyo hivyo kwa muda wa miezi 18
hatukupungukiwa,” anasema.
Baada ya hapo mwaka
2012, mtumishi wa Mungu alitupatia ukumbi wa ibada na ofisi Mabibo Gereji, barabara
ya Mandela, juu ya jengo la kituo cha Mafuta cha bure.
Hata hivyo, baada ya
muda wa miaka 3, tulipokea barua na mamlaka za nchi zinazoshughulika na mambo
ya mazingira. “Barua ilitaka tuondoe
kanisa katika maeneo ya biashara yake ya uuzaji mafuta vinginevyo asingeweza
kupewa leseni kamili ya biashara yake mahali pale kwa misingi ya kiusalama na
athari zinazoweza kutokana na moto”. Mwanzo tulishtuka, lakini tuliikubali
changamoto ile.
Hatimaye mwishoni mwa
mwaka 2013, tulianza maandalizi
kisaikolojia na maombi kwa ajili
ya ujenzi wa Kanisa. Mchungaji Dondo aliunda
kamati ya ujenzi Januari 2014 ambapo baadae Mungu alitusaidia kupata fremu ya
jengo la kanisa (Prefabricated structure) kutoka Marekani.
Kutokana na walengwa wa
huduma yetu kuwa wanafunzi hasa wa vyuo vikuu tulitafuta sana viwanja na kanisa
viwe karibu na wanafunzi.
“Tulitembelea viwanja
vingi maeneo hayo na gharama zilikuwa kubwa, vingi pia vilikuwa vidogo lakini
bei kubwa, tuliendelea tulimuamini Mungu kutupatia kilicho bora machoni pake”.
Baadaye, aliyekuwa Askofu
wa Mkuu wa TAG, Rev. Dk. Ranwell Mwenisongole ambaye ni Mchungaji Kiongozi wa
kanisa la TAG CCC - Upanga alituwezesha kupata kiwanja hiki cha Bahari Beach
ambapo sasa jengo limejengwa.
Usanifu wa Jengo la
City Harvest
Kiwanja cha City
Harvest kina kubwa wa mita za mraba 8,000 na jengo hilo lina ukumbi wa ibada wa
kukaa watu zaidi ya 1,000, vyumba vya madarasa vitano na ofisi za
wachungaji.
Nje ya jengo kuna nyumba
kwa ajili ya umisheni (Missions House) ambayo inatumika kwa ajili ya maandalizi
ya kwenda missions au ushuhudiaji au kufanya kambi za maombi.
Pia eneo lingine
limetengwa kwa ajili kiwanja cha michezo ambacho kwa sasa kipo wazi kwa ajili
ya watoto wote. Aidha huko mbeleni tuna
mpango wa kujenga shule ya awali (Nursery School) ya kimataifa ambayo tayari
iko kwenye matumizi ya mpango miji (land use plan).
City Harvest mpaka sasa
ina wachungaji wapatao 15. Kati yao wapo
wachungaji wanaotumika kanisani muda wote na wengine ni wachungaji washiriki
(Associate Pastors).
Kanisa la Kimisheni
City Harvest ni kanisa
la kimisheni, kwa miaka saba tumepeleka timu za umisheni South Sudan, Msumbiji,
Kigoma, Rufiji, Mkuranga, Bagamoyo, Lindi, Tandahimba, Kibaha (Bonde la Baraka),
Moshi na AfriKa ya Kusini.
Pia mwaka jana kwa
kushirikiana na jimbo la Dodoma Kusini (Mpwapwa) kanisa hilo lilifanikiwa
kupanda makanisa manne Winza, Chogola,
Chipogoro na Mtera katika mkoa wa Dodoma ikiwemo kununua kununua viwanja vine,
kujenga jingo la Kanisa moja na kutegemeza wachungaji saba kwa sasa. Tumeweza kununua kiwanja cha kanisa Lindi
mjini na tunao mpango wa kufungua kanisa India, ili kuwafikia wanafunzi wa vyuo
wa kitanzania wanaosoma huko. Tayari tumeshapata jengo Bangalore.
Mipango ya kanisa mwaka
huu ni kupanda makanisa mengine manne huko (Mpwapwa), kwa kuanzia kulingana na
mpango kazi aliotupa Askofu Mkuu. Kupitia kazi hii, Mungu ameibua vipawa mbalimbali
katika kanisa kama wainjilisti, waalimu na hata uzoefu wa ushuhudiaji, na mwili
wa Kristo umejengwa. Tunamtukuza Mungu.
Pia tumefungua tawi la kanisa kule Kigamboni ili kuwafikia wanavyuo wanaokaa
maeneo hayo na pia, tumeanzisha Bible Study, Haidary Plaza, ghorofa ya pili,
kila Alhamisa saa 11.30 jioni, kuwasaidia kujifunza maandiko wanaofanya kazi
katikati ya jiji na maeneo ya Posta.
Changamoto
Changamoto kubwa ya
kanisa inatokana na maono ya kanisa kuwa wanafunzi ni washirika wa majira na
nyakati. “Vyuo vikifunguliwa wanapatikana, vikifungwa wengi wanaondoka. Hivyo tunakuwa na muda mfupi wa kuwahudumia
pia wanapohitimu wanasambaa kutafuta ajira”
Pia Kanisa linahitaji
vifaa vya umisheni kwa ajili ya huduma za mikoani ambazo zinatawezesha
kuwafikia watu wengi kiurahisi.
Kanisa la City Harvest
linamshukuru Mungu kwa kufafanikisha kumalizia kazi ya ujenzi na mambo yate
makubwa ambayo yameonekana kipindi chote.
“Mungu ni mwema sana, hadi
sasa hatuna deni wala hatudaiwi na mtu au taasisi yoyote, Tumefanikiwa kuwa
huru kwa madeni”, anasimulia Mchungaji Dondo.
Kanisa la City Harvest
lilopo Bahari Beach pia limeanzisha huduma zinazoendelea kila Alhamisi saa 11
jioni katikati ya jiji kwenye jengo la Haidery Plaza na pia katika Kigamboni
kila jumapili kuanzia saa 10 alasiri eneo la Boat Beach, Maweni Mbuyuni.
Kwa mawasiliano na
kanisa la City Harvest, kwa maombi, maombezi na mengineyo, piga simu namba
0654320122 au tembelea ukurasa wa Facebook kujionea habari, picha, video na
mafundisho kwa kutafuta jina la City Harvest Church Dar es Salaam. Waweza pia
kuandika barua pepe kupitia anuani ya: cityharvestdar@yahoo.com
No comments:
Post a Comment