Friday, June 22, 2012

UTAMBUE UWEPO WA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO By Pastor Covenant at Christian Fellowship School of Social Sciences University of Dodoma - 18th June, 2012


Neno kutoka Yohana 1:1 – 4
“1. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye alikuwa Mungu. 2. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 4. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. (5. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza)”
-          Watu wengi wanakumbwa na mateso, maumivu na mahangaiko maishani mwao kutokana na kwamba Mungu hayuko katika masiha yao. Mambo hayo magumu yote yatakwisha mara tu mtu akitambua uwepo wa Mungu, kwani vitu VYOTE VILIFANYIKA KWA HUYO; WALA PASIPO YEYE HAKIKUFANYIKA CHO CHOTE KILICHOFANYIKA!
-          Neno alikuja kwa walio wake, wala walio wake hawakumtambua (laiti kama wangelitambua uwepo wake...!)
-          Kama mtu ukitambua uwepo wa Mungu kwenye maisha yako, utampa nafasi na kipaumbele pamoja na kumwamini katika mambo yote. Na ndiyo maana kitu kikubwa anachokifanya Ibilisi kwa watu ni kushika ufahamu wao ili wasitambue kabisa uwepo wa Mungu, kwani anajua wakiutambua, hana lake!
Katika kitabu cha Yohana sura ya 11, ndugu zake Lazaro walitambua kuwa kama Yesu rafiki yake angalikuwapo, basi Lazaro hangalikufa na ndivyo Martha dada wa Lazaro alivyomwambia Yesu (katika mstari wa 21). Hii inaonesha Martha alitambua kuwa katika uwepo wa Mungu, YOTE YANAWEZEKANA! Yesu alithibitisha nguvu za Mungu kwa kumwamsha Lazaro kutoka usingizi wa kifo, kwa sababu kwa Mungu vyote vinawezekana, na akiwepo katika maisha ya mwanadamu, YOTE YANAWEZEKANA
-          Kumbuka kuwa, PASIPO YEYE HAKIKUFANYIKA CHOCHOTE. Na hata Yesu amesema kuwa “Ninyi pasipo mimi hamwezi lolote” kwa hivyo njia pakee ya kuweza ni katika uwepo wake! Nayaweza yote katika Yeye anitiaye nguvu
-          Unaweza kujitahidi na kujiona kuwa na mafanikio katika maisha, lakini pasipo Yeye ni kazi bure.
Tunajua wazi kuwa giza haliwezi kuishinda nuru. Sehemu pekee giza linapotamalaki ni pale ambayo chanzo cha mwanga/nuru kimezuiwa. Kama ukizima taa kwa mfano, kutakuwa na giza. Lakini mara tu uwashapo taa, giza hutoweka mara moja.
Kama nuru imeweza kulishinda giza, wala giza halikuiweza, hivyo basi kama ukiwa na Mfalme wa Nuru basi ufalme wa giza hauwezi kukushinda. Kama ungekuwa na Yesu, mambo yote hayo magumu unayoyapitia usingeyapitia. Uweza, mamlaka na nguvu alizonazo Mungu si za kawaida, hashindwi na lolote lile. Nuru ingalikuwapo, giza lisingalikuwapo.
-          Shetani anatambua uwepo wa Mungu na hivyo pia kwa matatizo. Matatizo pia yanatambua nguvu za Mungu, na kwa kuwepo na Mungu katika maisha yako, matatizo hayatakuwa na sababu ya kuendelea kubaki, kwani katika uwepo wake hayawezi kuvumilia kukaa
-          Yesu ndiye ufufuo na uzima, ukiamini utauona utukufu wa Bwana (kumbuka alivyowaambia ndugu za Lazaro).
-          Hata kama matatizo yako yamechukua muda mrefu kiasi gani katika masiha yako, ukifikia hatua ya kutambua nuru inalishinda giza, uponyaji wako umefika tayari
-          Hata katika masomo yako, GPA yako pia itarekebishwa na ataishibisha! Unapaswa kutambua uwepo wa Mungu katika mfumo mzima wa maisha yako ya sasa na ya baadae. Hatupaswi kuishi tunavyoishi, bali kama vile Yeye alivyoishi. Ukifikia kuutambua uwepo wa Mungu, shetani hawezi lolote. Palipo na nuru giza halikai.
Mfano mmoja ni kuwa dada mmoja alikuwa karibu kuahirisha masomo yake ya chuo kutokana na masaibu yalikuwa yakimkuta. Alikuwa hawezi kusoma, akiingia darasani hamu yote inamtoweka. Lakini alipopata taarifa ya kuwa Mungu kupitia mtumishi wake amewezesha wengine, akaamini kuwa inawezekana na yeye kufanikishwa. Ilikuwa zimebaki siku mbili kabla ya mitihani kuanza, na alikwa haelewi afanye nini.
Nilimwambia dada huyo kuwa mimi niwe katika nafasi yake, naye awe katika nafasi yangu. Kitu nilichomuomba Mungu juu ya dada Yule ni kuwa “ninaomba ujuzi wa maswali yote, niwe na uwezo zaidi ya maswali na maswali yawe chini ya uwezo wangu, Amen” Hivyo tu! Dada alifurahishwa na maombi hayo na akapata nguvu za kusoma toka siku hiyo usiku mzima hadi siku iliyofuatia. Akaweza hata kusoma na mwenzake kamasehemu ya maandalizi ya mitihani.
Siku ya kwanza ya mtihani maswali aliyokutana nayo ni yaleyale ya sehemu alizozisoma. Alifurahi mno na hata kushindwa jina la kumuita Mungu (niliomba Roho wa Mungu amsaidie) kwani hatimaye yasiyowezekana kwa mwanadamu, kwa Mungu yamewezekana. Baada ya kumaliza mitihani vizuri akiwa na furaha na tumaini la mafanikio, aliuniuliza nifanyaje? Japo alikuwa mkristo wa madhehebu ya kiadventista, nilichomwambia ni kuwa ampe Yesu maisha yake.
Kupitia dada huyo ninamshukuru Mungu kwamba zaidi ya watu 30 wamevutwa kwa Mungu kwani yeye na familia yake walikuwa wakitoa machapisho kuelezea ushuhuda wao. Kwa sasa kitabu kinaandaliwa cha mkusanyiko wa shuhuda kinaitwa “MUNGU YUPO, NA NI HALISI”
-          Maneno ya kawaida na tuliyozoea kuyatumia, laity kama tungejua nguvu iliyoko ndani yake, basi tusingekumbwa na masaibu na taabu katika maisha. Mfano ni “Bwana Yesu Asifiwe”,  “Mungu akubariki” na mengineyo linapotajwa jina la Yesu uwepo wake hujaa. Tatizo ni kuwa hatutambui uwepo wa Mungu
-          Tatizo linalotokea kwako sasa usiwe na presha, kumbuka kama giza linavyotoweka taa ikiwashwa, ndivyo litakavyotoweka ukitambua uwepo wa Mungu. Kama mvua ishukavyo toka mbinguni,
-          Musa alitambua uwepo wa Mungu ndiyo maana pamoja na kuzungukwa na hatari pande zote (jeshi la Farao nyuma, mbele bahari ya shamu na pembeni jangwa) bado aliwatia moyo wana wa Israel kuwa wasiogope, watulie na watauona mkono wa Bwana. Na Mungu kwa nguvu zake aliwaokoa na kuliangamiza kabisa jeshi la Farao.
-          Zakayo pia alitaka sana kumuona Yesu kwa kutambua uwezo wake hata akapanda juu ya mkuyu, lakini Yesu alipomfikia alimwambia shuka mtini wokovu umefika kwako, na Zakayo alishuka na kumkaribisha nyumbani kwake. Kwa sababu ya uwepo wa Mungu katika maisha yake, aliwarudishia mara nne wale wote aliowadhulumu.
-          Neno la Mungu halitarudi bure, bali litatimiza mapenzi yake Yeye aliye juu

By Pastor Covenant
Email: covenantpastor@ymail.com

Sunday, June 10, 2012

CAREER'S DAY WORKSHOP TO BE CONDUCTED TODAY AT UDOM

LEO KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA SOCIAL SCIENCES KUTAKUWA NA WORKSHOP YA CAREERS DEVELOPMENT NA MADA KUU NI "ECONOMIC SITUATION AND LABOUR MARKET" AMBAYO INAANZA MUDA HUU SAA NANE MCHANA HADI SAA KUMI NA MBILI JIONI. WAZUNGUMZAJI WAKUU NI DK. CHARLES SOKILE KUTOKA DAR ES SALAAM NA WAHITIMU WA VYUO MBALIMBALI NA WADAU WENGINE WENGI. KARIBUNI SANA, NI SOCIAL SCIENCES THEATRE ONE.

JENGO LA KANISA TAG CITY HARVEST LAWEKWA WAKFU RASMI

HATIMAYE jengo Kanisa la TAG City Harvest limezinduliwa na kuwekwa wakfu na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, Rev. Dk. Barnabas Mt...