Thursday, January 26, 2012

NI MUHIMU KUJUA NYAKATI NA MAJIRA UNAYOISHI - by Azgard Stephen


NI MUHIMU KUJUA NYAKATI NA MAJIRA UNAYOISHI.
Namshukuru Mungu kipekee kwa kunipa nafasi hii ya kukuwekea somo hili. Nasema hivyo kwani inachukua muda kuandaa, ni lazima kuomba ili Mungu anipe ujumbe, lazima nifanye uchunguzi wa kina na pia kuuandika ujumbe katika 'internet'. Kwa hiyo si kazi rahisi, ni lazima kujitoa. Nikuhamasishe tu kwamba, upatapo ujumbe huu, mtumie na mwingine/wengine yeyote ili naye apate hii neema,ili kulijenga kanisa la Kristo.
UTANGULIZI.
Tunapozungumza kwa habari ya nyakati na majira tuna maana hii;
Majira: Ni vipindi mbalimbali ndani ya wakati ulioamriwa; mfano masika, kipupwe, kiangazi, n.k
Nyakati: Ni vipindi kulingana na matukio ya makusudi; mfano asubuhi, jioni, nyakati za mwisho, nyakati za utandawazi, wakati wa kupanda, kuvuna, n.k
Ni muhimu sana kufanya kila jambo kwa wakati namajira yake, mfano kupanda wakati wa kupanda, kuvuna wakati wa kuvuna, n.k
Siku zote ukifanya jambo nje ya wakati wake utaonekana kituko, na matokeo yake ni kutokufanikiwa. Kila jambo huonekana la busara mbele ya wenye hekima likifanyika ndani ya wakati wake, kwa lugha nyingine, "Everything is right at right time". Maana yake ni kwamba ukifanya jambo nje ya wakati hata kama jambo hilo ni jema, litabadilika kuwa baya. Wakati una 'impact' kubwa sana katika jambo lolote. Tazama formula ifuatayo;
1,000,000 * 0 = 0
·  Right thing* Wrong time = Wrong thing
·  Wrong thing * Right time = Right thing
·  Right thing *Right time = Right thing
·  Wrong thing * Wrong time = Wrong thing
Kwa hiyo unaweza kuona ni jinsi gani wakatiunavyoweza kuathiri mambo, hii ndiyo 'phylosophy'niliyo nayo. Kwa hiyo jambo ni jema sana likifanywa ndani ya muda wake. Kwa mfano, tendo lile lile linalofanywa na wanandoa likifanywa na watu ambao si wanandoa linakuwa si sahihi. Wala tendo halijabadilika, ni lile lile lakini kwa nini likifanywa na wanandoa ni sahihi na likifanywa na watu ambao si wanandoa sio sahihi? Tena limepewa na jina jingine kabisa, uzinzi; na ukifanya jehanamu unakwenda kwa miguu yote miwili. Tatizo hapa ni wakati!
Mhubiri 3:1-3
Hapa mwandishi anajaribu kutueleza kuwa kila jambo lina wakati na majira yake, tena kila kusudi. Anasisitiza kwa kuonesha mifano kadha wa kadha, wakati wa kuzaliwa, wakati wa kufa, wakati wa kupanda, wakati wa kuvuna n.k.
2Nyakati 1:7-10
Hapa tunamuona Sulemani anafanywa mfalme, akaona hekima na maarifa aliyo nayo hayamtoshi, yalikuwa yanamtosha wakati akiwa kijana, raia wa kawaida; ila wakati huu ni mfalme, hivyo akitazama kazi aliyonayo na kiwango cha hekima na maarifa aliyonayo, haoni uwiano. Mungu anamtokea na kumuuliza, "...omba lolote utakalo nikupe..." Mara Sulemani akakumbuka kiwango chake cha hekima na maarifa wakati huo, akamwambia Mungu, "...nipe sasa hekima na maarifa, nijue kuingia na kutoka mbele ya watu hawa..." Nataka uone jambo hili mahali hapa, si kwamba Sulemani hakuwa na hekima ama maarifa; alikuwa nayo, ila ya kujiongoza mwenyewe. Sasa wakati huu amekuwa mfalme, hivyo anahitaji hekima na maarifa ya kuwaongoza watu wengine.
Daniel 9:2,3
"...mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalitambua hesabu ya miaka, ambayo neno la Mungu lilimjia Yeremia nabii, ya kutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani miaka sabini."
Daniel anaposoma kitabu cha nabii Yeremia anatambua kuwa, wakati waliopo hawapaswi kuwepo Babeli, ila wanatakiwa kuwa wameondoka. Kilichokuwa kimeendelea kuwaweka Babeli ni kutokujua nyakati na majira ambayo wanatakiwa kuondoka Babeli.
Kwa hiyo baada ya Daniel kutambua kuwa walipaswa kukaa Babeli kwa miaka sabini ndipo akamlilia Mungu kumweleza kwamba wanatakiwa waondoke hapo. Kumbe kilichokuwa kinaendelea kuwaweka Babeli ni kutokujua wakati.
1 Nyakati 12:32
"Na wa wana wa Isakari , watu wenye akili za kujuaNYAKATI, kuyajua yawapasayo Israel wayatende; ... na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao"
Mungu alijua umuhimu wa watu wa namna hii,watu wanaojua nyakati, kujua wakati gani Israel wanapaswa kufanya nini. Tena Biblia inasema, kwa sababu tu ya wao kujua nyakati, "...ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao". Kwa hiyo ukijua wakati gani unapaswa kufanya nini, utakuwa na ujasiri wa kufanya mambo yako na siku zote utakuwa mtu wa kufanikiwa. Hii ni kwa sababu kila jambo chini ya jua hufanyika ndani ya wakati ulioamriwa, kulingana na mazingira husika. Na ndio maana leo ukikutana na mtu na kumuuliza kwa nini unafanya unachokifanya atakwambia 'nakwenda na wakati'. Ukijua ni wakati gani kitu gani kitatokea utajiandaa kukabiliana nacho.
Mathayo 26:36-46
Yesu alipojua ama alipotambua wakati wa kusulubiwa, alijiandaa kwa kufanya maombi mazito ya kuomba ujasiri wa kukabiliana na hali halisi iliyopo. Kama unafikiri natania, kasome mwenyewe utaona kuna wakati alisema "... kama ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke..." Kwa hiyo maombi aliyokuwa anayafanya, kwa kutambua wakati alionao yalikuwa na umuhimu mkubwa sana, na ni kwa maombi hayo ndipo malaika alishuka akamtia nguvu. Sasa fikiri kama asingejua kuwa huo ndio ulikuwa wakati wa kusulubiwa, halafu asiende kuomba; unafikiri huyo malaika wa kumtia nguvu ama moyo angempata wapi! Ukijua wakati gani unapaswa kufanya nini, utakaa katika eneo husika na utajiandaa kukabiliana na jambo hilo.
Nimekupa dondoo hizo chache za Biblia ili tu uone ni jinsi gani ni muhimu kujua na kutambua nyakati na majira unayoishi.
Nikueleze tu kwamba mafanikio yako ya kiroho na kimwili huendana sana na wakati. Watu hatufanikiwi kwa sababu tu hatujui ni zama gani tunazoishi sasa na tunapaswa kufanya nini. Kwa mfano, kipindi Yesu yuko duniani, yaani karne ya kwanza AD, ilikuwa mtu akiwa na gari linalovutwa na punda, ndiyo alikuwa anaitwa amefanikiwa, ama kwa maneno mengine yeye ni tajiri! Lakini mtu huyo huyo kwa kipindi chetu tunachoishi sasa si tajiri tena kwani mikokoteni ya kuvutwa na punda ni kwa ajili ya kukatia majani ya ng'ombe, kuchotea maji maeneo yenye ukame, kubebea samaki kwa wavuvi, kuzolea takataka kwa maeneo ya mjini, tena uswahilini,n.k. Mafanikio ni yale yale, lakini wakati! Kimsingi kabisa, kinachofanyika leo si kitakachofanyika kesho. Aina ya nyumba anayoishi baba yako leo sio aina ya nyumba utakayoishi wewe! Nizungumze sentensi ngumu kidogo, "kama kipato cha baba yako ni 500,000/= kwa mwezi kwa mfano, na wewe ukaja kuwa na kipato cha 500,000/= kwa mwezi, wewe na baba yako mtakuwa ni wapumbavu!" Sasa unaweza kuniambia kwamba mimi minekutukana,la hasha! Kimsingi ndivyo ilivyo kwani wakati anaoishi baba yako sasa sio wakati utakaoishi wewe, nyakati zinabadilika pamoja na mambo yake yote, hivyo ni muhimu kwa baba yako kukuandaa, na ni muhimu nawe kujiandaa kukabiliana na hali halisi ya wakati huo. Thamani ya pesa itabadilika n.k. Wakati nasoma Galanos, mwalimu wangu mmoja, mtu mzima kidogo, akaniambia kwamba, wakati anaanza kazi ya uwalimu miaka ya sabini, alikuwa analipwa mshahara Tsh. 400/= hivi kwa mwezi, na ni pesa ambayo ilikuwa inamtosheleza kwa mahitaji yake. Lakini kwa sasa analipwa zaidi ya Tsh. 150,000/=. Kazi ni ile ile, lakini mshahara wa wakati ule sio mshahara wa sasa; wakati!
MABADILIKO YA KIUCHUMI NA KISIASA TANZANIA
Miaka ya 1967 - 1985
Ni kipindi ambacho tulikuwa na siasa zaa ujamaa na kujitegemea. Zingatia mambo yafuatayo;
·  Thamani ya fedha ilikuwa juu kuliko sasa. Matumizi ya Tsh. 10/= kwa kipindi kile si kama ilivyo sasa.
·  Matumizi ama mahitaji ya watu yalikuwa chini sana ukilinganisha na sasa kwa sababu ya hali ya maendeleo ilivyokuwa
·  Wasomi walikuwa wachache na kiwango cha elimu kilikuwa chini ukilinganisha na sasa. Mtu wa darasa la saba aliajiliwa na serikali kama mkuu wa mkoa, waziri, n.k. Kwa mfano, waziri wetu mkuu wa kwanza, Kawawa, alikuwa na elimu ya darasa la nne tu, na alipewa jukumu la kuiongoza nchi. Sasa hivi hata kupewa kufagia ofisi za TRA huwezi.
·  Sayansi na Teknolojia ilikuwa chini mno, ni watu wachache mno walikuwa na magari ya kutembelea, computer hazikuwepo, na vitu vingi sana ambavyo unaviona leo.
Pamoja na hayo yote, mafanikio yalikuwepo, walikuwepo watu walioitwa matajiri kwa kipindi hicho, wakati!
Miaka ya 1986 - 1995
Huu ni wakati ambao watu huuita, kipindi cha ruksa. Watu binafsi walikuwa na pesa kuliko serikali. Watu waliacha kazi za kuajiliwa wakafanya biashara. Ilikuwa ni chini ya uongozi wa mzee Mwinyi. Zingatia yafuatayo;
·  Kiwango cha elimu kilianza kupanda, hivyo ajira zikaanza kuwabana watu wa elimu za shule ya msingi
·  Mzunguko wa pesa uliongezeka kwa kiwango cha juu, hivyo kuifanya pesa ianze kushuka thamani. Uchumi ukaanza kukua, watu wakaanza kuwa wamiliki wa mali.
·  Milango ilifunguliwa, bidhaa mbalimbali kutoka nje zikaingia nchini kwa kiwango cha juu kidogo
·  Mabadiliko ya kisiasa yalijitokeza, kulikuwa na mabadiliko kutoka 'monoparty' kwenda kwenye'multiparty' mwaka 1992, hivyo kubadili kabisa muelekeo wa siasa ya Tanzania.
Miaka ya 1996 - 2005
Huu ni wakati uliopewa majina mengi kidogo, zama za ukweli na uwazi, utandawazi, n.k. chini ya uongozi wa Mh. Mkapa. Zingatia yafuatayo;
·  Mambo yalibadilika kabisa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa mara ya kwanza bajeti ya serikali ikagomewa bungeni, wapinzani wote wakatoka bungeni, wabunge wa chama tawala wakaipitisha, mwaka 1996.
·  Mzunguko wa pesa uliongezeka pia kwa kipindi fulani, baadaye ukapungua kwa kuweka 'policies' mbalimbali kama vile 'monetary policy'.
·  Teknolojia imekuwa kwa kasi sana.
·  Kiwango cha elimu kimekuwa, wasomi wameongezeka hivyo kusababisha soko la ajira kuwa gumu.
·  Mawasiliano yamekuwa kwa kiwango cha juu pia.
·  Kumekuwa na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari na mawasiliano.
Sasa tuko miaka ya 2006 na kuendelea, chini ya uongozi wa Mh. J.M. Kikwete, mambo yanayoendelea kulingana na zama hizi zinazoitwa zamaa za maisha bora kwa kila Mtanzania wewe ni shahidi, ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, utakuwa na majibu sahihi kabisa.
Nia na madhumuni ya kukupitisha katika hayo nataka tu uone tunakotoka na tunakokwenda, ili uweze kujua unapaswa kufanya nini. Kulingana na mifano hiyo ningetamani ujifunze mambo yafuatayo;
·  Mabadiliko ya kisiasa yanavyoathiri hali ya maisha ya watu na muelekeo wa nchi, hivyo unapaswa kufanya nini kulingana na hali hiyo. Unaweza kusema kwani siasa zitaniathiri nini, lakini angalia kipindi cha ujamaa, hata kuuza maandazi binafsi ilikuwa hairuhusiwi, kila kitu duka la ushirika, hakukuwa na uhuru wa kutoa maoni kama ilivyo leo, siasa!
·  Mabadiliko ya kiuchumi na jinsi yanavyoathiri maisha ya watu; kwa mfano, kutoka 'socialistic economy' hadi kufikia 'mixed economy'. Ni jinsi gani mabadiliko hayo yameathiri hali ya uchumi ya watu na taifa kwa ujumla. (kumbuka athari zaweza kuwa positive ama negative)
·  Mabadiliko ya sayansi na teknolojia na jinsi yanavyoathiri hali halisi ya maisha ya watu, hivyo ufanye nini.
·  Hali halisi ya kiroho na muelekeo wa kanisa kutokana na mabadiliko hayo, ama kulingana na nyakati zinavyobadilika. Kwa mfano, maadili kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, wewe kama kijana ufanye nini ili kulinda hali yako ya kiroho.
·  Kasi ya maendeleo na mabadiliko hayo, kwa kipindi gani mabadiliko yametokea, na yaliyopo sasa
Nikupashe tu habari kwamba, usitegemee, kwa mfano wewe ni mwanafunzi wa chuo kikuu, hali ya soko la ajira kwa sasa itakuwa hivi hivi hapo wewe utakapomaliza, la hasha! Tazama kitu unachosoma, tazama soko lake kwa sasa, tazama uhitaji (demand)wake kwa sasa, angalia ni wasomi wangapi wako chuo kikuu wanaosomea kitu hicho, tazama idadi ya wale waliopo kazini, angalia kasi ya kukua kwa'population' mwisho angalia uhitaji (demand) wa kitu hicho kipindi wewe utakapomaliza chuo na miaka utakayokuwa kazini. Unaweza ukasema sasa nitajuaje, nikueleze tu kwamba 'statistics' zipo, tena kwenye internet, hivyo ni wewe tu kuwa makini na kutafuta hayo mambo. Tatizo tulilonalo watanzania ama waafrika kwa ujumla, tunaishi kwa ajili ya leo tu, kesho atajua Mungu. Lakini hiyo sio njia sahihi ya kuishi, na ndio maana Mungu aliweka watu wa kujua mambo yajayo Israel.
Kwa mfano, nchi kama Marekani, wanatengeneza'computers' ziatakazokidhi mahitaji ya mwaka 2015, yaani wanaitazama 2015 leo kabla hata hawajafika. Wanatazama mfumo wa uchumi wa kipindi hicho leo, wanatazama mahitaji ya watu mwaka 2015 leo. Lakini huku kwetu leo kuna watu wanatumia 'computers'window 2001 na bado hawajamaliza kutumia 'programmes' zilizomo.
Nikueleze tu kwamba, kujua unakoelekea ni muhimu kuliko hata kujiandaa, kwani unaweza ukajiandaa sana, lakini muda ukafika hicho ulichojiandaa hakitumiki tena. Kama unafikiri nakutania, kasomee kutengeneza 'type-writers' sasa hivi, halafu uwe unategemea kuja kufanya kazi kama 'engineer', yaani kukamilisha masomo yako mwaka 2020 uone kitakachokutokea. Nasisitiza kwamba, ni muhimu sana kuangalia soko la kile kitu unachofanya leo kwa miaka utakayokuja kukifanyia kazi, ni muhimu sana. Kwa mfano, kwa sasa kuna wanafunzi wengi sana wanasoma sheria, wengi mno. Lakini mimi nikiangalia tunakokwenda, soko la ajira katika sheria na wanafunzi walioko vyuoni hakuna uwiano, hivyo ni dhahiri kwamba kuna watu wengi sana, wasomi, ajira itakuja kuwa kitendawili kwao, hivyo itawapasa kuja kujiajiri wenyewe. Sasa kujiajiri mwenyewe si tatizo, tena ni jambo jema sana, lakini je huyu mtu amejiandaa kujiajiri? Maana kitakachotokea ni maandamano, ajira hakuna! Sasa sikukatishi tamaa usisome sheria, ila nataka tu uone unakoelekea na ujiandae kukabiliana na hali utakayoikuta huko.
Kuna watu wanafanya mambo siku za leo wakidai wanakwenda na wakati, lakini kimsingi hawaendi na wakati ila wanafanya mambo yaliyopitwa na wakati. Kwa mfano, siku moja muinjilisti mmoja alikuwa nahubiri, akawauliza wakina dada kwa nini wanapakaa wanja; wenyewe wakadai wanakwenda na wakati. Yule muinjilisti kawaambia, "Mngejua kwamba huyo aliyeanza kupaka wanja alifanya hivyo miaka 700 kabla ya Kristo, na alikuwa ni Yezebeli, mke wa Ahabu, ambaye alikuwa mwanzilishi wa mungu Baali, na anaitwa mama wa makahaba, msingepaka wanja kwa kudai mnakwenda na wakati!" Nimekupa tu 'challenge' ujue ukifanya kitu unakifanya kwa misingi gani. Sasa sikwambii usipake wanja, hasha! ila tu ni muhimu kujua kwa nini unapaka wanja!
Kama Mungu akinipa nguvu, nitakutumia mfululizo wa pili wa somo hili unaohusu nyakati za mwisho, yaani kurudi kwa Masihi kulichukua kanisa na kitu gani kitajili baada ya hapo. Usikose kufuatilia. Kama nikisahau, nikumbushe, ama fuatilia katika e-mail hii,watumishi07@yahoo.com kwa kutumia password hiimaombi. Neema ya Mungu ikufunike na Roho mtakatifu akuwezeshe kuyaelewa haya.
Ev. Azgard S.Chamulungwana
sheghwede@yahoo.com
+255713990607

JENGO LA KANISA TAG CITY HARVEST LAWEKWA WAKFU RASMI

HATIMAYE jengo Kanisa la TAG City Harvest limezinduliwa na kuwekwa wakfu na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, Rev. Dk. Barnabas Mt...